Basi chupa ile ya Wine iliyorushwa na Joy ileenda na kutua moja kwa moja katika mkono wa kushoto wa Joy na kumjeruhi damu zikaanza kumwagika. Lakini pia zile kelele alizopiga Joy kutokana na woga pamoja na maumivu ya kujeruhiwa na chupa aliyoirusha Joy iliwafanya watu wengine waliokuwemo ndani ya chumba cha V.I.P kupata mshtuko na kusogea eneo la tukio kushuhudia kilichoweza kutokea.
Wengi walioshuhudia tukio lile walighadhabika sana na kutoa lugha mbalimbali zisizo na shule lakini pia wapo walioona kama ni tukio la kawaida kwa mazingira kama yale. Wenzie na Joy pia hawakuwa mbali kwani nao walighadhabika sana kiasi cha kutaka kuzua ugomvi mkubwa dhidi ya Joy na Boss France lakini haikuweza kuwa rahisi kwani Mabamnsa waliokuwa wakihakikisha usalama wa pale V.I.P walishafika na kuanza kutawanya watu. Erick mmoja wa Mabamnsa wa V.I.P alimgonga, gonga begani ili kutaka kumpooza Boss France aliyeonekana kuwa a hasira zaidi juu ya Joy kwa kufanya kitendo kile na kibaya zaidi ni Baada ya kutambua kuwa yule alikuwa ni Vicky mmoja kati ya wafanyakazi wake katika idara ya uhasibu.
Vicky aliendelea kulia sana kwa uchungu kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata ikambidi Boss France aliyekuwa akilengwalengwa na machozi ikiwa ni ishara tosha ya kupata hisia za kushea maumivu ya Vicky kwa kiasi fulani kuchukua jukumu la kumbembeleza Vicky kwa kumpapasa mgongoni kwa mikono yake huku akitoa maneno ya kumpa Vicky matumani na faraja mpya. “Dear Vicky nafahamu ni jinsi gani unahisi maumivu makali na uchungu mkubwa juu ya tukio hili, lakini usijali kwani mimi niko hapa kwa ajili yako na nitahusika kwa kila kitu zikiwemo gharama za matibabu yako ili kuhakikisha unarejea katika hali yako ya kawaida”. Naye Vicky hakuwa mchoyo wa shukurani na tabasamu dhidi ya Boss France alijibu “Asante Boss kubwa sasa nahisi kufarijika” ingawa Vicky alikuwa katika maumivu makali baada ya kujeruhiwa mkono wake wa kushoto na Joy aliyemrushia chupa tupu ya Wine.
Hakukuwa
na mjadala wa kuendelea kuwepo pale HAVOC NIGHT
SPOT CLUB kwani Vicky alitakiwa kupelekwa kwa ajili ya kupata
matibabu. Naye Boss France hakutaka kuendelea kumuona Vicky akivuja damu kwani
alichukua kitambaa chake alichokuwa nacho mfukoni na kumfunga Vicky katika
mkono wake uliokuwa umejeruhika. Alifanya hivyo huku akiendelea kumpa matumaini
Vicky aliyeonyesha kuanza kulegea kwa kukosa nguvu.
Boss France aliendelea kumsisitiza Vicky kwamba asihofu punde tu atarejea katika hali yake ya kawaida. Boss France alijikakamua na kumbeba Vicky katika mikono yake ili kumpeleka katika gari lake kwa ajili ya kumuwahisha Hospital kwa ajili ya kupata matibabu na mmoja kati ya mabamnsa waliokuwepo pale alionyesha ushirikiano kwa Boss France kwa kutaka kumbeba Vicky aliyekuwa tayari katika mikono ya Boss France kitendo cha kumpeleka Vicky katika gari kilikuwa nicha haraka kwani alikuwa amembeba Vicky huku akichanyanga miguu kama injini iliyofungiwa mota.
Hatimaye
alimfikisha Vicky katika gari yake na kulaza siti za nyuma ili kumruhusu Vicky aweze
kupumzika huku akiwa amenyoosha miguu yake. Wakati huo Boss France alitamani
aweze kupata mtu mwingine ambaye angemsaidia kuendesha gari lake kuelekea
hospitali ilihali yeye aweze kukaa karibu na Vicky ili kuendelea kumpa faraja. Hakuwa
na budi kumuomba Erick mmoja kati ya mabamnsa waliokuwa mule V.I.P ili
kumsaidia kuendesha gari kuelekea Hospitali.
Erick hakuweza kusita kwani tukio hilo lilikuwa nila dharura ilimbidi atoe msaada wa haraka na wakati hayo yote yakiendelea naye Joy aliyekuwa sababu ya matatizo yote hayo alikuwa mita chache kutoka kwenye gari la Boss France huku akiachilia kilio kilichosindikizwa na machozi na kuonyesha majuto juu ya uamuzi wake ulioweza kuleta tafrani.
Erick alikamata usukani huku akiendelea kusikiliza maelekezo kutoka kwa Boss France aliyemtaka kukimbiza gari haraka kuelekea AGA KHANI HOSPITAL iliyoko maeneo ya posta pia ikiwa si mbali sana na eneo lao wanalofanyia kazi. Basi bila ya kigugumizi Erick alikuwa akiendesha gari kwa mwenda wa kasi mithili ya Ambulance kiasi kwamba alikuwa akikatisha bila ya kusimama katika baadhi ya maeneo ya Barabara. Kulikuwa na mwendo kidogo lakini iliwabidi kuelekea AGA KHANI HOSPITAL sehemu ambayo ingekuwa na uangalizi wa salama zaidi kwa Vicky.
Kwa bahati nzuri gari la Boss France lilikuwa likijitosheleza kwani pia lilikuwa na box maalumu kwa ajili ya huduma ya kwanza. Hivyo wakati safari ikiendelea Boss France alilazimika kutoa huduma ya kwanza kwa Vicky aliyekuwa akilalama juu ya maumivu ya jeraha “Aaaah...aiiisiiiii” alilalama Vicky aliyeonekana kujilegeza na kugaragara juu ya miguu ya Boss France ambaye aliganya kazi ya kutoa huduma ya kwanza kwa Vicky. Nyakati zilikuwa zimekwisha kwenda sana kwani muda huo ulikuwa ni wa majira ya saa saba na nusu usiku. Ghafla Boss France aliwaza juu ya shughuli za ofisi kwani kukucha kwa usiku huo kulimpasa Boss France kuendesha kikao cha wakuu na wasaidizi wa vitengo mbalimbali ndani ya Hyatt Regency Hotel.
Lakini
ilikuwa ni ngumu kwake kupata majibu sahihi kwamba kipi kitajiri wakati
utakapofika ikiwa ilimpasa kujali sana kuhusu Vicky kama alivyokwisha kumpa
ahadi ya mapema. Baada ya kitambo kidogo waliwasili katika Hospital ya
Aga Khani na kupokelewa kwa dharura na wahudumu waliokuwa shifti ya
usiku. Walikaribishwa na kupewa pole na mmoja wa madaktari aliyekuwa na jukumu
la kuchukua uangalizi dhidi ya wagonjwa wao kwa usiku huo.
Daktari
huyo alikuwa ni Dr. Adamu ambaye alikuwa ni msaidizi wa Dr. Mkuu na Rafiki wa
karibu wa Boss France aliyefahamika kwa jina la Dr. Justine. Huyu alikuwa ni
moja wa marafiki wakubwa wa Boss France na mmoja kati ya watu wakarimu sana
katika Hospital ya Aga Khani. Wahudumu walimchukua Vicky na kumpeleka moja kwa
moja kwenye chumba cha kulaza wagonjwa, wakati huo Boss France alikuwa akihaha
na kuzunguka kulia na kushoto kwa kuhitaji Vicky aweze kupata matibabu ya
haraka sana. Kichwa chake kilionekana kujawa na mambo mengi ndani ya mda mmoja
akiwa na mashaka zaidi juu ya Vicky, aliwaza
na kuwazua huku akisubiria uamuzi wa Daktari kwamba ni kipi kingeweza kuendelea
kuhusu Vicky.
Ingawa
alishaanza kuhisi uchovu lakini ilimpasa kuendelea kuvumilia ili kuhakikisha Vicky
anakuwa salama. Alijaribu kuvuta picha juu ya tukio zima la usiku huo na
kujiona kuwa ni mtu mwenye ugundu ndani yake na wakati akiendelea kufanya hivyo
ghafla sauti ya Dr.Adamu ilimwondoa katika mawazo yale na kumtaka kuingia ndani
ya ofisi yake ili kuweza kujadili jambo kidogo.
Dr.Adamu alimkaribisha Boss France ndani ya ofisi yake na kutaka kujua juu ya lile lililomkuta Vicky naye Boss France alieleza mwanzo mwisho wa tukio lile. Baada ya Dr.Adamu kupata maelezo alimwambia Boss France kwamba hali ya Vicky siyo mbaya na wala si njema sana kwani tayari alikuwa amekwisha kupoteza kiwango fulani cha damu lakini alimwakikishia kumpatia matibabu ya kina. Boss France aliuliza juu ya nani ambaye angeweza kuwa mwangalizi wa karibu wa Vicky kwa usiku huo lakini Dr.Adamu alimtaka aondoe shaka na kumwambia kwamba Hospital yao inatoa huduma za kimataifa na imejikamilisha kwa kila idara. Basi alimuomba Dr.Adamu aweze kumruhusu kwenda kumuaga Vicky kabla ya yeye kurejea nyumbani kwake kwa usiku ule. Dr. Adam aliridhia hilo na kuongozana moja kwa moja katika chumba alichokuwa amelazwa Vicky.
Aliingia ndani na kumtizama Vicky nayo machozi yalianza kumtoka kwa kumuona Vicky akiwa katika hali ile. Alimsogelea na kuketi pembezoni mwake pale kitandani na kumtaka radhi juu ya lile lililotokea kisha akamuaga na kumtaka asihofu kwani angeweza kupata matibabu na huduma zote na Kumhakikishia usalama wa kutosha.
Wakati huo Vicky hakuweza kuzungumza lolote lakini ghafla alimshika mkono Boss France wakati alipotaka kusimama na kuondoka Looh..! Boss France alishtuka naye Vicky aliendelea kusisitiza kwamba hawezi kubali Boss France aondoke kwa usiku huo na kumtaka yeye ndo achukue uangalizi dhidi yake na wala si mwingine. Dr. Adamu alikuwa akishuhudia tukio lile na kushindwa kutoa tamko lolote lile zaidi ya kubaki kuwakodolea macho.
Vicky
alimshikilia kwa nguvu Boss France kwa mkono wake wa kulia na kutaka kujaribu
kukaa lakini Dr.Adamu alisogea kutaka kumzuia asifanye vile kwani alipaswa
kuendelea kupumzika zaidi. Lakini naye alizuiliwa na mkono na Boss France
ambaye alimtolea jicho la ukali na kumtaka kumwacha Vicky afanye alichojisikia
ingawa alikuwa akiwaza zaidi juu ya kikao cha asubuhi ya siku hiyo. Alifanya
vile ili kumzuga Vicky apate usingizi na yeye kuweza kuondoka endapo hilo
lingefanikiwa. Ghafla Vicky aliishiwa nguvu tena na kupoteza fahamu
ghafla huku akijiachia na kuanguka kitandani. Boss France na Dr. Adamu
walishtuka huku wakitoa macho nje kwa sauti za “Mama
yangu” huku kila mmoja akitaka
kuwahi kumzuia Vicky asije akagongesha kichwa sehemu ya ukutani.
****MWISHO****
Je, ni kipi atakachofanya Boss France kati ya kuendelea kubaki Hospital kwa ajili ya uangalizi dhidi ya vicky au kuondoka kuelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kupumzika na kujiandaa kwa ajili ya kikao cha kiofisi cha asubuhi ya siku hiyo?
0 Comments