A story by Sebastian Masabha
0758-162527
Boss
France aliendelea kumkumbatia vicky, wakati huo Esther aliyekuwa akiendelea
kudondosha machozi yake nyuma ya Boss France alikodoa macho kwa nguvu zote ili
kujaribu kumfahamu mwanamke aliyekuwa amekumbatiana na Boss France. Dkt Justine
na jopo lake la madaktari na manesi nao hawakuwa na chakufanya zaidi ya
kuendelea kuwatizama Vicky pamoja na Boss France wakiwa wanabadilishana joto la
miili yao. Esther hakuwa tayari kuendelea kukubaliana na hali ile aliyokuwa
akiishuhudia mbele ya macho yake kwani alisogea karibu na kuwavaa akina Boss
France pamoja na Vicky.
La
hasha!.. naye Dkt Justine alijikuta akiropoka “Hapana, hapana Esther
usifanye hivyo” lakini Esther
hakujali juu ya kauli ya Dkt Justine kwani wimbi zito la wivu wa kihisia juu ya
Boss France lilishamvaa na kujitoa fahamu kwa lolote lile mahala pale. Dkt
Justine aliendelea kufoka “Wewe Esther ina maana haujui kwamba
mimi.......” kisha akasita kuendelea kuzungumza na kuanza kujigonga,
gonga kichwani mwake Looh!.. ama kweli ilikuwa ni vita ya
waziwazi ya kihisia iliyokuwa ikimtesa kila mmoja kiasi cha kusema “unachokikataa
wewe mwenzio kina mnyima usingizi” kwani yalikuwa ni mapigo ya mpigiko yaliyoupiga
moyo wa kila mmoja.
Haikuwa
rahisi kwa Esther kuelewa wala kumsikiliza yeyote yule zaidi ya Boss France kwa
wakati ule kwani ndiye aliyekuwa tazamio lake pasipo ya Boss France kuligundua
hilo. Esther alishtushwa kiasi cha kwamba ilimbidi harudi hatua mbili nyuma
baada ya kutambua yakuwa mwanamke aliyekuwa amekumbatiana na Boss France
alikuwa ni Vicky. Alifyonza kwa nguvu na kwa kejeli “Mfyuuuu....Mshenzi
mkosa akili, kumbe ni wewe mwanamke mpenda hanasa” alitoa maneno hayo
ya kejeli huku akimtizama Vicky kwa kumpandisha na kumshusha mara tatu tatu kwa
macho yake ya asali.
Vicky
hakujali kuhusiana na kejeli zilizokuwa zikimtoka Esther katika kinywa chake
kwani naye alimtizama Esther kwa dharau na kisha akaupeleka mdomo wake na
kumpiga kisi zito Boss France aliyekuwa haelewi upande wa kulia ni upi na wala
upande wa kushoto ni upi kwa wakati huo.
Baada
ya hatamu fupi wakiwa bado pale Hospitali Boss France alipigiwa simu na mtu
aliyeshindwa kumtambua kwa wakati huo. Simu hiyo ilipigwa na mtu aliyetanguliza
salamu za pole kwa Boss France kutokana na madhila yaliyomkuta na kumfanya
kuwepo pale AGA KHAN HOSPITAL kwa muda wa siku kadhaa. Mazungumzo baina ya Boss
France pamoja na mtu huyo yaliwafanya akina Esther, Vicky, Dkt Justine na wengine wote waliokuwa katika
eneo hilo wakae kimya na kuendelea kusubiri juu ya kile kilichokuwa kinaendelea.
“Habari Boss! Pole na madhila yaliyokusibu na kupelea kushindwa kuendelea
na shughuli za kulijenga taifa kwa siku kadhaa” mtu huyo alizungumza na
Boss France pasipo kuweka utambulisho wake lakini alionekana kuwa ni mtu
aliyemfahamu vema Boss France. “Ahsante sana ndugu lakini napata wasi
kujua naongea na nani” alihoji Boss France kutaka kufahamu alikuwa
akizungumza na mtu gani. “Naitwa PRINCE ALPHONCE ni mkaguzi mkuu wa makampuni
na mashirika ya umma na yasiyo ya umma hapa nchini, nimefanya mazungumzo na wewe ili kupata kibali
cha kutembelea Hoteli yako yenye hadhi ya NYOTA tano kikazi zaidi.” Alijitambulisha
mtu huyo na kupata ukaribisho mzuri kutoka
kwa Boss France ambapo waliafikiana kwamba ugeni huo utapaswa kuwasili
siku mbili mbeleni.
Haikupita
hata dakika Boss France akapigiwa simu tena kwa njia ya Whatsapp video call na
mmoja wa wafanyakazi wake Waooooh... Ilikuwa ni suprize kwake kwani alichokiona
katika kioo cha simu yake lilikuwa ni jopo la wafanyakazi wenzake kutoka katika
idara tofautitofauti wakiwa na shauku ya kutaka kufahamu hali aliyokuwa nayo Boss
wao kwa wakati huo.
Zilikuwa
ni nyuso mbalimbali zilizoonyesha tabasamu murua kwa kufurahi kuona Boss wao
akiendelea vema. “Hi.. Boss we miss you.. so much..” ilikuwa ni
sauti ya mmoja wa wafanyakazi wake aitwaye Nice aliyeshindwa kuzuia hisia zake
kwa kummiss Boss wao kwa siku kadhaa. Esther alimgeukia Dkt. Justine na kutaka
kujua juu ya gharama za malipo ambazo kampuni ingepaswa kugharamia juu ya matibabu
ya Boss France. Wakati akihoji hilo naye Boss France alidakia na kuchomekea neno.
“Je vipi kuhusu Vicky? kwani hautambui yakwamba naye alilazwa hapa kwa
siku kadhaa” Heeh!... Jambo hili lilionekana kuwa jipya kwa Esther
ambaye hakuwahi kufahamu lolote lililomkuta Vicky na kupelekea kuwa pale
Hospital. Esther akaanza kujiuliza na kujisemea katika moyo wake na fahamu zake
“Alaah inawezekanaje ya kwamba Vicky alikuwa amelazwa hapa siku zote hizo
pasipo ya mimi kuwa na taarifa”.
Kisha
akatikisa kichwa na kuendelea kujihoji “Ahaah! Sasa nimehisi kitu nadhani
ndo ile siku niliyopigiwa simu asubuhi na Boss France na badae akataka
kuniambia juu ya jambo fulani alafu akasita ahaa! Nadhani ndivyo nimeshapata
majibu” pamoja na hayo yote na kutokana wimbi la wivu wa kihisia
lililokuwa likizidi kumpanda kichwani mwake akaona aendelea kujipa maswali na
kukujibu ili kuiridhisha nafsi yake. “ Sasa kwanini Boss France
akuniambia?, kwanini anifiche? na wakati
mtu alipata matatizo au alihisi nitamvurugia kwa Vicky? haaaah! Kumbe Boss
France atakuwa anampenda sana Vicky. Je,
vipi watakuwa wameshafanya lolote lile lakini hapana maana Vicky alikuwa
ni mgonjwa Huhuhuu.. Mimi sijui bhana ngoja niyaache” Baada ya Boss
France kumhoji jambo Esther na kuona ukimya umetawala aliamua kumuita “Wewe
Esther unawaza nini mbona kama akili yako haipo hapa? Akaongezea tena
kwa mara nyingine Vipi kuhusiana na Vicky Je, kampuni haimtambui? Esther alishtuka
na kutoka katika lile wimbi la mawaza na akaona kwamba alichokuwa akikiwaza ni
ujinga mtupu.
Kampuni
itahusika Boss wangu ila kwa vielelezo maalumu vinavyoonyesha chanzo cha yeye
kuwepo hapa maana kama kampuni hatukuwa na taarifa ya Vicky na wala wewe
hukuwahi kunijuza chochote kuhusu kulazwa kwa Vicky hapa Hospital. Baada ya
majibu hayo Boss France aliona kwamba hakuna haja ya yeye kuendelea kuitaka
kampuni ihusike na gharama za matibabu ya Vicky kwani kuendelea kufanya hivyo
kungesababisha Esther pamoja na wafanyakazi wenzake waweze kutambua siri nyingi
katika yake yeye na Vicky. “Basi naona itakuwa ni prosesi sana hivyo mimi
binafsi nitagharamika na gharama zote za matibabu za Vicky zilizosalia” alijiwahi
Boss France kusema hivyo huku akiwa na lengo lake kichwani wa kutaka kuepusha
mlolongo wa mambo yaliyojificha.
Baada
ya Dakika kadhaa bili zote za matibabu ya Boss France pamoja na Vicky zililetwa
na mmoja ya wafanyakazi waliokuwa wakihusika na kitengo cha uhasibu pale Hospitali
kutokana na Amri ya Dkt. Justine. Alikuwa ni mdada aliyekabidhi bili zote mbili
za matibabu kwenye mikono ya Boss France. Boss France hakuweza kusema chochote
zaidi ya kutoa ghuno na kukaa kimya huku akimtizama yule Dada machoni mwake. Boss
France alipaswa kulipa kiasi cha Milioni tatu kama sehemu ya gharama
zilizotumika kumtibu Vicky. Wakati huo gharama za matibabu yake zikiwa ni
Millioni nne na laki tisa kitu ambacho akikuweza kusumbua kichwa chake kwani
kampuni ndo ilipaswa kugharamika juu ya matibabu yake.
Alichukua
bili ile na kumpatia Esther huku mkononi mwake akiwa na bili ya matibabu ya vicky.
Kwa wakati huo aliona ni ngumu kuondoka na kwenda kuchukua kiasi hicho cha pesa
mahala alipo zihifadhi, ikambidi kumpigia simu mmoja wa marafiki zake wakubwa
na Boss mwenzake aliyekuwa ni Meneja katika Hotel kubwa ya SERENA HOTEL ambayo
nayo ipo katika orodha ya Hotel zenye hadhi ya NYOTA tano Jijini Dar-es-salaam.
Boss huyo alifahamika kwa jina la Meneja Tinno maarufu kama sultani ambapo lilikuwa
ni jina alilopachikiwa na wafanyakazi wenzake kutokana na mwonekano wake wa
kufuga ndevu nyingi zilizokuwa zimejitapakaza hadi mashavuni mwake mithili ya
mzee mkavu.
Boss
Tinno kwa kutambua umuhimu wa rafiki yake mkubwa na ambaye wamekuwa
wakishindana pakubwa katika kuzitangaza na kuziendeleza Hotel zao za NYOTA tano
kama mameneja hakuwa na budi kumuagiza mmoja wa madereva wake kufikisha kiasi
hicho cha pesa AGA KHAN Hospital. Esther aliandika hundi yenye malipo
yaliyohitajika kulipia matibabu aliyofanyiwa Boss wake na wakati huo naye
dereva wa meneja Tinno alikuwa akiwasili na kiasi cha pesa alichoagiziwa
kumfikishia meneja Tinno.
Walifanya malipo na kisha wakaagana na
kumshukuru Dkt.Justine na timu yake kwa msaada na uangalizi wake mpaka kupona
kwa wagonjwa wao.Baada ya zoezi hilo iliwabidi waanze safari ya kuondoka kurejea majumbani mwao
maana muda nao ulikuwa umeshasonga sana. Ilikuwa imeshatimu mishale ya saa kumi
na mbili jioni. Esther aliafiki kwamba yeye angefanya jukumu la kumpeleka Boss
France nyumbani kwake Oyster bay na kushauri kwamba angefanya pia jukumu la
kumkodishia Vicky taks ambayo ingempeleka moja kwa moja hadi nyumbani kwake.
Loooh.... Hapo Esther alikuwa ni kama amefanya kazi ya kuumwagia moto petrol
kwani Vivky alimuangalia jicho baya utadhani alitaka kummeza mzima mzima.
Lakini wakati hayo yakiendelea naye Dkt.
Justine alikuja mkuku mkuku huku na bila ya kufikiria ya kwamba Esther alikuja
na gari lake pale akaropoka “Mimi nitamdindikiza Esther mpaka nyumbani
kwake na Boss France wewe utakwenda pamoja na Vicky” ikabidi wote
wabaki kumtizama kwa kuona kama Dkt. Justine alikuwa amepagawa na kuhisi kwamba
pengine yawezakuwa kuna kemikali zimemchanganya. Boss France alimshika Vicky na
kumvuta pembeni ili kumnong'oneza jambo fulani naye mzee wa mikurupuko
aliyechanganyikiwa kihisia na uwepo wa Esther akajaribu kumshika Esther mkono
lakini loooh.. haikuwa kama ilivyokuwa kwa Boss France na Vicky kwani
alikutanishwa na kofi la uso kutoka kwa Esther lililowashtua pia Vicky na Boss
France na lililofanya miwani ya Dkt. Justine ianguke chini na kujishika uso
huku akibakia kusema Lah! Lah! Lah!...
***MWISHO***
Endelea
kufuatilia miendelezo ya tamthiliya hii
ili kupata mafunzi na burudani maridhawa
A story by Sebastian Masabha
0758-162527
0 Comments