Esther
alishuka kwenye gari lake na kapanda ngazi mkuku mkuku kuelekea katika ofisi ya
Dkt. Justine. Alifika mlangoni akagonga mlango lakini hakukuwa na ishara wala
sauti yeyote aliyoweza kumkaribisha ndani, akaendelea kugonga mlango ule mpaka
mara tatu na kimya nacho kikaendelea vilevile ikabidi afungue mlango na kupenyeza
kichwa chake ndani ili kuona kama palikuwepo na mtu. Alishtuka kidogo baada ya
kuona yakuwa hapakuwa na mtu ndani, ikambidi atoke na kwenda kwenye ofisi ya Dkt.
Adamu na kisha akafanya kama alivyofanya kwenye ofisi ya Dkt. Justine lakini
kwa bahati mbaya ofisi ya Dkt. Adamu ilikuwa imeshafungwa.
Punde
tu, aligeuza shingo yake na kutizama kulia na kushoto bila ya kuweza kuwaona
wahusika wake na hapo akarudisha mawazo nyuma kukumbuka kwamba alimwacha Grace
pale Hospital kwa ajili ya kumpa taarifa juu ya Boss wake Boss France.
Alichukua simu yake kutoka katika mkoba
na kisha akaipigia namba ya Grace lakini pia haikuwa bahati kwa muda huo
kuweza kumpata Grace kupitia njia ya mawasiliano ya simu kwani simu yake haikuwa
hewanikwa mda huo.
Lakini
alibaki akijiuliza kwamba angeweza kumpata wapi, lakini kwa bahati nzuri wakati
akiyawaza hayo kwa mbali aliweza kumuona Dr. Justine akirejea katika ofisi
yake, naye hakutaka kupoteza muda ikabidi amfuate hukohuko.
Wakati
akitembea kwa haraka haraka na kufika nje ya mlango wa ofisi ya Dkt. Justine
kisha akauzuia mlango ambao ulikuwa ukifungwa na Dkt. Justine aliyekuwa
akiingia ndani ya ofosi yake. “Kefule!!!... Nini tena?, Ahaah! Kumbe ni wewe karibu sana” alizungumuza
Dkt. Justine, mithili ya mtu aliyejiuliza na kujijibu mwenyewe. “Asante
Dkt. Justine” aliitikia Esther ambaye alikuwa katika hali ya kutaka
mambo yake yaweze kwenda kwa uharaka. “Dkt. Vipi kuhusu hali ya mgonjwa
wangu nahitaji kufahamu hilo” aliuliza Esther huku akimtizama Dkt. Justine katika macho yake. “Unapaswa
kusubiri mgonjwa wako atakuwa sawa tu” alijibu
Dkt. Justine huku akionyesha hali ya kutokujali sana juu ya Esther. Maskini Esther
alishusha pumzi kidogo kutokana na jibu la Dkt. Justine na kisha akaupeleka
mkono katika blauzi yake na kulegeza kifungo kimoja cha juu huku akijipepea kwa
tishu nyepesi.
Madoido
na mitego ya Esther kwa Dkt. Justine haikuishia hapo kwani alianza kuyachezesha
macho yake huku akidai kwamba palikuwa na Joto mule ndani licha ya Viyoyozi vyote
vya ofisi ile vikiwa vimewakwisha kuwashwa.
Dkt.
Justine alizidi kuhamaki na hakuamini juu ya kile kilichokuwa kikifanywa na Esther
na hapo alipeleka mawazo na akili yake mbali zaidi kwa kuhisi kwamba siku hiyo ingeweza
kuwa siku ya bahati ya mtende kana kwamba aliona ni kama amekwisha kuliokota Dodo
chini ya mti wa mkwaju.
Esther
aliendelea kumpagawisha na kumuhamisha zaidi Dkt. Justine kwa kitendo cha
kulamba lamba midomo yake huku tabasamu lenye ladha ya mwani wa kipwani
likimtoka. Eboooh! Dkt. Jastine alikuwa akimwangalia tu Esther
huku akishindwa kuzungumza jambo lolote lile. Dkt. Justine alianza kushusha
miwani yake na kuining'iniza chini ya macho yake kisha akaanza kujichekesha chekesha dizaini
ya mlevi aliyeona chupa ya balimi mbele ya macho yake, wakati huo eneo la zipu ya suruali yake
ilianza kupanda juu kama rocket iliyotaka kupaa angani. Na hapo Esther akaanza
kuamini yakuwa mtego wake alianza kufanya kazi kikamilifu.
“Dkt.
Justine” kukawa
kimyaa... “Dkt. Justine” kukawa Kimyaaa tena, Kisha Esther akaamua kugonga meza kwa nguvu na
kuita tena kwa mara ya tatu “Hey! Wewe Dkt. Justine” naye Dkt.
Justine akakurupuka dizaini ya mtu aliyeamshwa kutoka usingizini. “Naam
naam ndiyo nipo Mwalimu” Kheee!!! Esther akamshangaa Dkt.Justine na
kucheka kidogo kisha akaamuliza “Mwalimu wako katoka wapi tena hapa” naye
Dkt.Justine hakuweza kujibu chochote hapo zaidi ya kuendelea kumtizama Esther.
Esther
aliyeweza kuziteka fahamu za Dkt. Justine ndani ya sekunde chache mithili ya
delila wa samsoni, Esther alianza
kujisifu na kujifurahia ndani ya moyo wake kwamba uzuri wake ndio ulioweza
kuyafanya hayo yote. Esther alizidi kujikweza na kujisifu zaidi baada ya kupata
mwanzo mzuri na mwepesi kwake kwa kufanikiwa kuutambua udhaaifu mkubwa wa
Dkt.Justine ambao kwake ungekuwa ni fimbo na silaha ya kuweza kufanikisha
matakwa yake.
“Dkt. Justine bila shaka ulinipigia simu na kuniuliza ya kuwa nilikuwa wapi” alihoji Esther naye Dkt. Justine akakimbilia kujibu kwa pupa bila ya kufikiria “Ndiyo nilitaka nikuone” na hapo Dkt. Justine alijiingiza katika kesi isiyomuhusu mithili ya mbuzi aliyejitwika mafiga ya moto. Dkt. Justine alijikuta akilikubali swali la Esther na wakati hili suala lilikuwa nila Dkt. Adamu ambaye alimpigia simu Esther na kuitelekeza ofisi yake na kukimbilia Restaurant baada ya kuliona gari ya Esther likiwasili pale hospital.
Ilikuwa ni ishara tosha yakwamba Dkt.Justine alikuwa amekwisha jifia katika moyo ya Esther pasipo kujitambua, Dkt. Justine alijikuta akimpa Esther ushirikiano mkubwa juu ya Boss wake. Walitoka nje ya ofisi na kuelekea alipokuwa amelazwa Boss France Looh!!!.. Naye Esther alishindwa kuweza kujizuia kwa kukimbilia pale kitandani kwa Boss wake na kuanza kulia kwa machozi ya furaha baada ya kumuona Boss wake akianza kurejesha fahamu zake zilizokuwa zimetoweka siku kadhaa baada ya ile ajali.
Dkt. Justune aliakuwa akimkata jicho
Esther huku karoho kawivu kakianza kumtawala,
alijisikia vibaya kwa kuhisi kwamba mapenzi ya Esther yalikuwa
yakijidhihirisha kwa Boss France. Wakati hayo yakiendelea kusawidi mara ghafla Boss
France akaanza katamka maneno yaliyokuwa hayaeleweki zaidi sana kwa Esther. Boss
France alianza kutamka maneno hayo huku akigaragara pale kitandani “Huuuu... Huuuu...Nakuja, nakuja kukuchukua tuondoke naimani ushapona kwani
nimekusubiri sana kwa muda mrefu” Looh!!! Na hapo Esther alijikuta akiyabadili
machozi yake yaliyokuwa ya furaha na kuwa yenye uchungu mkubwa hata pia manesi
waliokuwa pale nao walijikuta wakipata huzuni juu ya tukio hilo.
Lakini
ilikuwa ni tofauti sana kwa Dkt. Justine ambaye yeye hakuweza kuonyesha hali
yoyote ya masikitiko juu ya jambo lile. Dkt. Justine aliweza kulitafsiri jambo
lile kwa haraka na kuhisi ya kuwa Boss France alikuwa akiwazia sana juu ya
Vicky ambaye anaye alikuwa ni mgonjwa aliyelazwa hapo hospital bila ya hawa
Esther na wengine kufahamu hilo. Hii ilikuwa ni siri kwa Dkt. Justine ambaye
alifurahia ile hali na kuona yakuwa ingekuwa ni rahisi kwake kuweza kumpata
Esther aliyekuwa amekwisha kumteka moyo wake mazima.
Esther
alizidi kulia kwa uchungu huku akiwa amepiga magoti yake na kumsihi Dkt.
Justine aweze kufanya lolote juu ya hali ya Boss France. Na hapo Dkt. Justine hakuwa
na ubishi kwani hakutaka kuyaana machozi ya Esther yaendelee kumtoka. Alitoa
maelekezo kwa madaktari wadogo na manesi kwamba ni nini wafanye ili kuhakikisha
hali ya Boss France inahimarika mara moja. Ikabidi Dkt. Justine na Esther
kutoka nje ili kuwapisha wahudumu kuweza kuhangaikia hali ya Boss France.
Dkt.
Justine alikuwa akimgongagonga bega na kumpooza Esther kwa kumpapasa katika
mgongo wake kwa lengo la kumtuliza kuacha kulia kwani hali ya Boss wake lazima ingeweza
kuwa sawa kwa uangalizi wake. Aliendelea kumbembeleza Esther na kumsihi
waelekee katika ofisi yake ili akapumzike, Lakini ilikuwa ni tofauti kwa Esther ambaye
hakuwa na haja ya jambo hilo. “Oooh!!! Bila shaka utakuwa haujala basi
naomba tuelekee Restaurant kupata chakula pamoja” alizungumza Dkt.
Justine ambaye alikuwa akishusha pumzi yake “Huuuh...”... huku akimtizama
Esther kwa jicho la uchu wa kutaka kukubaliwa ombi lake. “Hapo
umejiongeza kama mwanaume unayejitambua lakini asante nimeshiba na sihitaji
chochote kwa sasa”.
Dkt.
Justine alihisi kuishiwa na pozi kwani wakati Esther alipoanza kutoa jibu lake
lilionekana kuanza kumpendeza na kumfurahisha lakini ghafla likawa na kona
iliyoidhohofisha furaha yake. “Basi naomba twende ukapate chochote
utakachokihitaji” alizungumza huku akitabasamu lakini majibu ya Esther.kwa
mara nyingine hayakuweza kuuridhisha moyo wake “Sihitaji chochote kile
Dkt. Justine” hayo ndiyo yaliyokuwa majibu ya Esther na yenye nyodo na
ishara za dharau kwa Dkt. Justine.
Esther alikuwa akiyafanya hayo yote huku akiwa
na uhakika kwamba Dkt. Justine. asingeweza kumfanya chochote wala kushindwa kuacha
kumsaidia Boss France kwa kuwa alikuwa akimpenda yeye. Ilikuwa imekwisha timia
majira ya saa nane mchana na baada ya
kimya kidogo masikio ya Dkt. Justine yalisikia kupata ladha ya vanila katika
ulimi wa mtu aliyetafuna mwarobaini, kwani Esther alikubali kwenda Restaurant
pamoja na Dkt. Justine.
Furaha
ilishamiri tena kwa Dkt. Justine na kuonyesha tabasamu kisha wakaanza kuelekea Restaurant.
Lakini kabla hata hawajapiga hatua mbili tatu, Dkt. Justine aliitwa na mmoja wa
manesi ambao walikuwa wakitoa matibabu kwa Boss France. Nesi huyo alikuja alipokuwa
Dkt. Justine na Esther huku akikimbia na kuonekana kuwa mwenye furaha baada ya kuirejesha
hali ya Boss France. Suala hilo lilikuja na taswira mbili kwani ilikuwa ni
zaidi ya furaha kwa Esther ambaye aligeuka na kukimbilia kule alipokuwa Boss
France huku naye Dkt. Justine akikimbilia huko huko ingawa moyo wake ulikuwa na
manung'uniko kwani jambo lake alikuweza kufanikiwa na ndo kwanza lilikuwa
katika hatua za awali.
Esther
aliingia moja kwa moja mpaka kwenye chumba alichokuwemo Boss France bila ya
kujali taratibu zozote na kwenda kumkumbatia Boss France aliyekuwa amekaa pale
kitandani Waaaoooh!!!.. Iliendelea kuwa ni furaha isiyo na kifani kwani naye
Boss France aliita “Esther, Esther” baada ya kumuona kisha wote wakatabasamu huku machozi ya
furaha yakimtoka tena Esther. Wakati hayo yakiendelea Dkt. Justine na wengine
waliokuwepo pale walibaki kuwa mshuhuda wa tukio lile la kihisia.
Likini
ghafla Boss France alikumbuka juu ya Vicky ambaye naye alikuwa amelazwa pale
hospital ikiwa yeye mwenyewe ndiye aliyemleta hapo na kumahidi juu ya usalama
wake na kila kitu kabla ya yeye kukumbwa na ajali. “Mamaaa....!!!” Alikurumuka
pale kitandani na kuchomoa drip aliyokuwa ametundikiwa katika mkono wake kisha
akakimbia kuelekea katika wodi aliyolazwa Vicky. Kheeh!!!.. Ulikuwa
ni mshangao na mshtuko kwa kila mmoja pale kasoro tu kwa Dkt. Justine ambaye
alikuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
Boss
France aliinia katika wodi aliyolazwa Vicky na kumkuta amesimama kwa kujiandaa
kuondoka pale hospital huku akiwa pamoja na jopo la wale marafiki zake aliokuwa
nao kule HAVOC NIGHT SPOT CLUB kabla ya kulazwa kwake hapo
Hospital. Waooh!! Aliachilia simu yake aliyokuwa ameishika kutaka
kumpigia Boss France na kumkumbatia Boss France kwa muda mrefu huku akiangua na
kilio cha maumivu ya kupotezana na mbaya zaidi ni pale alipomwona Boss France
akiwa na majeraha katika mwili wake.
Wakati
huo Esther, Dkt. Justine na lile jopo la
madaktari na manesi lilikuwa likikimbilia huko huko huku Esther akiwa wakwanza.
Baada ya kufika mlangoni na kutupa macho yake mbele alibahatika kumuona Boss
France akiwa amekumbatiana na mwanamke ambaye alikuwa amegeukia upande wa pili
na yeye kushindwa kumtambua. Looh!!!.. na hapo Esther aliendelea kulia kwa
sauti huku akiita “Boss France,
Boss France”
MWISHO.
Je,
ni nini kitakachoendelea baada ya tukio lile la Esther la kumkuta Boss
France akiwa amekumbatiana na mwanamke aliyeshindwa kumtambua kwa haraka?
Endelea kuwa nasi katika sehemu zinazoendelea.
MWANDISHI
SEBASTIANI SEBA
PHONE: 0746445197

0 Comments