PENZI LA MASHAKA
A STORY SCRIPT BY
SEBASTIAN S MASABHA. 0758-162527
SEHEMU YA KWANZA 01.
GETONI UNGA_LIMITED ARUSHA
(USIKU)
SEBBY ANARUDI GETONI USIKU BAADA YA KUTOKA KWENYE MIZUNGUKO YAKE YA
MAISHA.
SEBBY.
Oyaa! Red fungua mlango jembe langu, Oya
mwamba fanya kuchangamka si unajua tena mtaa wetu. Usiku huu.
{Red anaamka kwa kujinyoosha na
kumfungulia mlango Sebby}
RED.
Dah! Vipi chafu yangu, mbona leo umechelewa
sana alafu kama kinyonge, umefua dafu kweli huko kitaa?
SEBBY.
Sijui hata nianzie wapi kukueleza ndugu yangu
maana ni majanga matupu. Yaani ni madhila yaleyale tu kama ilivyo torati.
RED.
Pole sana ndugu yangu. Ila napata shaka
kidogo maana leo umepoa kinoma.
SEBBY.
Kwanini mwamba?
RED.
Siyo Stella yule shemeji yangu mzua matatizo
kila kukicha ama Sabrina mtoto wa kishua ndo anakuchanganya.
{Sebby anashtuka kwa kusikia habari za
Stella na Sabrina anamgeukia Red na kumjibu kwa ukali}
SEBBY.
Haah! Upuuzi huu sasa, unazungumzia kuhusu
nini? Stella ama Sabrina. Hakuna cha Stella wala Sabrina hawahusiani kabisa na
mambo yangu.
RED.
Sawa, samahani ndugu yangu hauna haja ya
kuchukia wala nini, haya ni mambo ya kawaida sana. Embu kwanza funua bakuli
hapo kwenye kijimeza chetu upate walau chochoye kitu.
{Sebby anafunua bakuli lililopo juu ya
meza na kuhamaki}
SEBBY.
Alaah! Mshkaji wangu kumbe ni mihogo na
samaki perege. Umetisha sana maana sikutegemea.
RED.
Ndo hivyo tukipatacho dua tu ndugu yangu
maana maisha yetu kwa sasa na mafanikio bado ni mbingu na ardhi.
SEBBY.
Ila kweli mwamba maana wewe ndiye unayeniweka
mjini mara zote na urafiki wetu hauna kikomo kwani tunaishi zaidi ya ndugu
sasa.
RED.
Sahihi kabisa chafu yangu, basi wewe endelea
kupata.
{ Sebby anaanza kula mihogo na samaki perege}
SEBBY.
Sema kitu kimetulia mwamba, lakini hili giza na mende waliopo humu ndani, wananifanya
nikumbuke ile hadithi ya “mzee tola anakula
gizani”
RED.
Hahahaa.. mshkaji wangu umenikumbusha mbali
sana. Yaani enzi hizo tulikuwa watoto wadogo mno. Basi ngoja nikuwashie kibatari
upate walau mwanga kidogo.
{ Red anaingiza mkono wake chini ya
uvungu ili achukue kibatari}
RED ( V.O )
Aiiiii.... chichichi.... Asee mama yangu.
Aah! Kulaleki.
SEBBY.
Eeeh! Vipi tena mwamba.? Mbona yowe kama
zote.
{ Sebby anatoa simu yake mfukoni haraka,
anaiwasha na kumulika uvunguni}
SEBBY.
Lalalala! Pole sana mwamba. Kumbe ni “Nge”
ndo amekunyatua.
RED.
Shukrani sana ndugu yangu. Nadhani atakuwa ni
“Nge” maana napata maumivu fulani ya kibingwa. Yaani ameniwaru kinyama.
SEBBY.
Ngoja nikusaidie jembe langu sababu maumivu
yake siyo poa. Mara ya mwisho mimi kung’atwa na “Nge” ilikuwa ni miaka mitano nyuma
tena alikuwa ni mdogo kama huyu. Huwa Wanang’ata sana hawa.
RED.
Asee.. ni kweli chafu yangu. Alafu nashangaa
“Nge” mpaka kwenye hiki kipindi kisicho cha mvua.
{ Sebby anachukua kiwembe na kutoa sarafu
ya mia mfukoni ili amfanyie Red huduma ya kwanza }
SEBBY.
Sasa jikaze mwamba nikufanyie matibabu ili
sumu isienee mwilini.
RED.
Poa mshua wewe fanya yako ya kitabibu zaidi.
{ Wakati sebby akiendelea kumfanyia Red
huduma ya kwanza simu yake inapokea ujumbe (sms) kutoka kwa Sabrina }
( Sabrina sms )
“Hello! Good night
my Gentleman. I’ love you”
{ Sebby anausoma ujumbe ule na kujibu
kibabe kisha anaendelea kumfanyia Red matibabu }
( Sebby sms )
“Poa nashukuru”
{ Sebby anamchana Red kidogo sehemu aliyong’atwa
na kumwekea sarafu juu }
SEBBY.
Hadi hapa tushaua mwamba. Sasa inabidi
upumzike na maumivu yataisha yenyewe maana hicho kijax kitavuta maniaje yote.
RED.
Dah!
Jah bless you. Umetisha sana chafu yangu. Sema nini ujue kabla sijasahau yule
Bi. Mdashi si katimba leo kudai kodi yake. Yaani sielewi hata tunafanyaje.
SEBBY.
Bhanaee.. wewe temana nae. Yule Bi. Mdashi huwa ni mzinguaji
kinoma. Kwani anatudai shingapi mpaka sasa?
RED.
Anatudai Elfu hamsini.
Si unajua tumelimbikiza sana. Alafu mbaya zaidi katupa siku tatu tu
tusipokamilisha, anatufurumushia vitu vyetu nje.
{ Sebby anakosa
ujanja kwani anapoa na kujibu kinyonge }
SEBBY.
Mmmh! Elfu hamsini
parefu na hii hali yetu. Ila wewe usijali pumzika mimi nitajua ni kipi cha
kufanya.
{ Red anaamua kuvuta shuka lake na kulala.
Sebby naye anajiegemeza kitandani na kuwaza }
SEBBY.
Kusema kweli kuipata Elfu hamsini ndani ya
hizi siku tatu ni kipengele. Maana pesa ya kula tu yenyewe ni Mungu saidia tu.
{ Baada ya muda
mfupi Sebby anapitiwa na usingizi na kulala }
NDANI GETONI (ASUBUHI)
SEBBY ANASHTUKA KUTOKA USINGIZINI
{ Sebby anashtuka na kujinyoosha kisha
anamuamsha rafiki yake Red }
SEBBY.
Mwamba, Mwamba, Oya Mwamba.
RED.
Vipi tena chafu yangu kuamshana usiku. Kwani
Kuna nini?
SEBBY.
Acha ndoto za usiku bhana. Tizama dirishani
pashakucha. Kwanza vipi unajisikiaje.
RED.
Kweli ya leo siyo ya jana. Angalau najisikia
poa.
SEBBY.
Hapo sawa. Basi wewe endelea kupumzika, wacha
mimi niingie mzigoni. Si unajua ile kauli ya biashara asubuhi, jioni mahesabu.
RED.
Poa chafu yangu. Namimi nikipata ahueni sitolaza
damu nitaibuka huko mara moja tupambanie Jax.
SEBBY.
Usijali wewe leo jipe tano tu za nguvu wala
usihangaike Kabisa. Mezani hapo nimekuachia jero utaenda kushtua utumbo kwa
Mama Chepe.
RED.
Poa ndugu yangu. Ndo maana wao wanakuita
chafu yao na mimi nakuita chafu yangu haujawahi niangusha hata siku moja.
{ Sebby anatoka nje, ananawa uso na
kuondoka kuelekea sinoni daraja mbili kwenye gereji anayofanyia kibarua }
Fade out.
NJIRO NYUMBANI KWA KINA SABRINA
(ASUBUHI)
SABRINA ANAAMKA ASUBUHI HUKU MAWAZO YAKE YOTE YAKIWA JUU YA SEBBY
{ Sabrina anaamua kushika simu yake na
kumtumia sebby ujumbe (sms) }
( Sabrina sms )
“Hello dear Sebby, It's my pleasure you doing well. Usiku wa leo nimelala nikikuota hata
visivyoelezeka. Inshort am speechless my love”
{Sebby Akiwa Njiani Anapokea Ujumbe Wa Simu
Kutoka Kwa Sabrina. Anasimama pembeni ya barabara anausoma na kujisemea
kichwani mwake}
SEBBY. (V.O)
Yaani huyu naye asubuhi- asubuhi tu anawaza
mapenzi na siyo kingine. mida ya kufanya kazi hii. Alafu Mtoto mwenyewe wa
kishua sasa mimi na yeye ni wapi na wapi.
{Sebby Anaacha Kujibu Ujumbe Ule Na Kuendelea Na Safari Yake. Anatembea kwa muda kidogo na kufika gereji wa kwanza, kisha anabadili mavazi yake na kuvaa vazi la kazi. (Overall ) }
SINONI_DARAJA_MBILI_GEREJI (ASUBUHI).
{Kabla Ya Kuanza Kufanya Chochote Sebby
Anapokea Ujumbe Mwingine Wa Simu Kutoka Kwa Stella}
( Stella sms )
“Kipenzi nimekumisi, alafu si
unajua leo kuna sherehe ya shosti angu huku mtaani, hivyo nitumie pesa ya
kusuka”
{Sebby anaangalia ule ujembe wa simu kutoka
kwa stella. Anatamani kuupotezea kulingana na hali yake mbaya ya kifedha, lakini
kwa kuwa anampenda hana budi Kumjibu
japo Kinyonge }
( Sebby sms )
“Sawa, ujumbe wako nimeuona. lakini
hivi kweli mpenzi wangu Stella ndo hamna hata cha salamu. Anyway poa nikipata
nitakutumia kwa sasa nipo kibaruani”
{ Sebby anaanza tena kujilaumu kwamba ni
kwanini ameahidi kumtafutia stella pesa ya kusuka ilihali mambo yake bado
hayajakaa sawa }
SEBBY.
Hivi huyu mwanamke kaniloga ama, yaani
namkubalia kirahisi rahisi hivi wakati hapa sina hata mia ya kusingiziwa na
tunadaiwa kodi. Eeh! Ama kweli mapenzi ni upofu ila haya yangu ndo funga kazi
kabisa.
ITAENDELEA....
N.B- USISAHAU
KUDONDOSHA COMMENT YAKO NI MUHIMU
PIA USIKOSE KUFUATILIA MIENDELEZO YA TAMTHILIYA MBALIMBALI KUTOKA KWA MTUNZI NA MWANDISHI SEBASTIAN S MASABHA
1.PESA ZA SHEMEJI
2. KONEKSHENI ZA VALENTINE
3. SUKARI YA KIJIJI

0 Comments