Kuna nyakati katika maisha inaibidi ujiachilie mbele ya mwenyezi mungu ili uweze kupona,

Tatizo la watu wengi wanataka kumwonyesha mungu kuwa wanauzuni kila siku, hakuna siku ambayo  wanataka au unataka kumwonyesha mungu kuwa unafuraha. Kwa mfano chukulia una rafiki au ndugu yako kila akikuona ni kilio na hakuna siku inabadilika. Ilo ni tatizo.

Wengi wetu tunakumbukumbu za zamani ambazo zinatusumbua maishini. Inawezekana chanzo ikawa:-
Malezi; inawezekana ulikosa malezi Fulani kutoka kwa wazazi wako na unapojaribu kwendana na jamii inayo kuzunguka inashindika ndipo majina mengi unapewa kwa sababu unashindwa kufit na jamii usika mfano wa majina hayo kama mskini jeuri, kaza roho na mengineyo.  Kutokana na majina hayo na kushindwa kuendana na jamii una mwomba mungu ufanikiwe ili uje kufundisha adabu. Ilo kwa mwenyezi alitakiwi utabaki hivyo miaka yote.
Mahusiano yaliyovujika;  mwanamke au mwanume uliye mwacha unatamani umpate  mwingine zaidi yake ukamwonyeshe sasa una mzuri zaidi yake. Au tokea uhusiano wa kwanza uliovyo vujika haujawaipata uhusiano ulio tengemaa na kila mara unapo kumbuka uhusiano wa nyuma unatamani kurudi ila inashindikana.
Shida iliyotokana na uhusiano. Kwa mfano ugojwa; tokea kipindi icho unajuta. Yaani  ulivyo kuwa kwenye mahusiano mmoja wenu kamwambukiza ugojwa Fulani. Tokea siku hiyo ulivyo jua ukajenga chuki
Upizani wa ki siasa, kiuchumi na kielimu na  kila ukikumbuka  unajiona umepoteza (loser).
Kufiwa na mzazi mmoja au wote na ukikumbuka waliokufanyia mazuri unabaki unalia na unjihisi kushidwa. na mengineyo mengi yanayo sababisha kumbukumbu mbya  maishani 
‘Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kumbukumbu mbaya katika maisha’  maana kumbukumbu mbaya usababisha malipizi na vifungo vya nafsi.

Njisi ya kupona kumbukumbu mbaya maishani
kwa kupitia BIBLIA TAKATIFU tunapata njia ya kupona kabisa kumbukumbu mbaya maishani

Isaya 43:18-19
Neno la mungu linasema
“18 Msiyasubukie mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani.
19 tazama nitatenda neno jipya, sasa liatachepuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito nyikani.”

Mungu anaweka katazo kabisa la kuyakumbuka mambo ya zamani na haikubaliki licha ya ata kuyatafakari.Tena ukisoma mstari wa 19, Mungu mwenyewe  anakupa njia nyingine na atatenda mengi makuu ata kama upo kwenye shida.
Biblia hituambii ni mambo ya zamani au  leo au kumbukumbu nzuri au mbaya,  ila neno kumbukumbu alikubaliki katika maisha ya binadamu.
Hivyo basi
“Hauwezi kuishi kwa harufu ya pilau jana”
Ndugu zangu katika bwana tutafakari maneno haya katika maisha
Kufa ni rahisi kuliko kuishi.
Kuanguka ni rahisi kuliko kuinuka.
Kushidwa ni rahisi kuliko kushinda.
Kurudi nyuma ni rahisi kuliko kwenda mbele.
Kusema nimechoka ni rahisi kuliko kusema nina nguvu
Kushi katika maisha ya jana ni rahisi kuliko kuumba maisha mapya.

Tafakari
Kwa nini wana waisraeli walichelwa jangwani?
Au  kwa sababu walikuwa wanakumbuka vitu na maisha ya misri?

Lazima tuache kumbukumbu mbaya au nzuri ziende kwa  mfano kuna msemo mmoja wa waswahili unasema ‘yaliyo pita sio ndwele tungange yajayo  awa jamaa walijifariji tu wenyewe japo hawana mungu.
“Angalia mbele kuna mambo mengi zaidi ya Baraka”

Zaburi 79:8
Neno la Mungu linasema
8 usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu,  rehema zako zije kutulaki hima, kwa maana tumethirika sana.

Daudi ana mwomba mwenyezi mungu asikumbuke maovu baba zetu sisi wanadamu. Ila kinyume chake rehema zake mungu zije kutubariki.

Isaya 43;25
Neno la Mungu linasema
25 Mimi, naam, ndimi niyafutaye makosa  yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.
Mungu ndiye afutae makosa yetu  na wala atazikumbuka dhambi zetu, Mungu ni Mungu wa haki at any given time.

Waebrania 8:12
Neno la mungu linasema
12 kwasababu nitawasamehe maovu yao, na dhambi zao sitazikumbuka tena.

Ivyo ndivyo njisi gani Mungu wetu alivyokuwa na nguvu, Kama yeye anaweza kufuta kumbukumbu mbaya na dhambi zetu, kwa nini sisi tushindwe kufuta kumbukumbu mbaya wakati tumeumbwa kwa mfano wa Mungu.
Unaweza ukitaka
“Only if you willing you can”
“Stop complaining about past start doing what is, now”
“It’s time to keep moving”