Matokeo ya picha ya jump in another stage in life


Ndugu zangu; wapendwa katika bwana, tunapenda sana tufanikiwe tuwe na maisha mazuri ila tunashindwa kusonga mbele kwa sababu ya HOFU”

Hawezi kupenya katika maisha hasa  ki biashara bila kudiriki kupenya dhidi ya hofu
Katika maisha tunayo ishi kuna aina kuu mbili ya hofu
1 Hofu nzuri chini ya uhuru
2 Hofu mbaya chini ya vifungo

Nitazungumzia ki ufupi hofu nzuri maana lengo langu ni kuzungumzia hofu mbaya chini ya vifungo vya nafsi.
Hofu nzuri chini ya uhuru inaweza ikawa juu ya usalama nyumbani (hapa unaweza kuweka kitasa nyumabani kwako, security camera, pia walinzi wa nyumba), hofu nzuri ya kumjua mungu na kuacha dhambi na tamaa za ulimwengu.
Hofu mbaya chini ya vifungo
Sababu za hofu mbaya maishani (kibiashara)

  1. Kukosa elimu sahihi        
  2. Kukosa taarifa sahihi
  3.  Kukosa ujuzi sahihi 
  4. Kukosa Maarifa
Watu wengi tunashindwa kuthubutu katika biashara mbalimbali sababu ya  hofu. Hivyo  basi ni vigumu sisi kusonga mbele  tuna fanya kazi kwa ulegevu na kutokuaamini kama utafanikiwa. Siku zote; mtu mwenye mafanikio tena anafanya kazi yake bila hofu. ata neno la mungu  katika mithali 10:4 linasema  hivi  atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; bali  mkono wake aliye  na bidii hutajirisha


Lengo langu ni kukutia moyo kwamba usikate tamaa na usiogope ATA NENO USIOGOPE LINATAJWA MARA 360 KWENYE BIBLIA (ina maana, siku moja ina neno moja)

Aina ya hofu mbaya
1 HOFU YA KUCHUKUA HATUA AU MAAMUZI MAGUMU JUU YA MAENDELEO, UWEKEZAJI, KUFANYA BIASHARA
Hofu hii imekamata au kutawala hasa kwa vijana wa sasa , wanaogopa kufanya biashara waskiogopa kwamba wataanguka na kushindwa kusonga mbele.
Lakini hayo yote yanasababishwa na ukosefu sahihi wa elimu, ujuzi, taarifa, maarifa,  juu ya biashara unayo taka kufanya
Hata ukichukua mkopo, ukakosa maarifa, ujuzi, taarifa na elimu ni vigumu kufanikiwa
Kama ukichukua mkopo fanya mambo yafutayo yatakusaidia na kusimama imara ki biashara.

  1.               Usichukue mkopo ukakimbia benki
  2.              Jenga jina vitu vidogo vidogo
  3.              Kopa na rudisha mkopo upate uhaminifu

Nataka nikukutia moyo hasa kwa wale wano kopa pesa na  wanao  anza biashara, maana maneno yanakuja ili kukuthohofisha na kukukatisha tamaa na kukutia hofu mfano Fulani kashindwa je wewe utaweza?.
2 HOFU YA KIFO, WEZI, WACHAWI
Hofu ya kifo
Hauwezi kufanya au kutenda mema, kufanya vitu vya maendeleo kwa sababu una hofu kuwa ukiwa tajiri utakufa mapema.
Hofu ya wezi
Hawezi kununua vitu vizuri kama magari, vitu vya ndani una hofu ya kuibiwa, pia hofu ya kuongeza bidhaa kwenye duka au maduka yako.
Hofu ya wachawi
Hapa ndio tatizo la wengina linatutesa wengi, yaani unashidwa kutumia mali zako vizuri sababu ya wachawi watakuloga.
Njisi ya kuvuka ni kutulia na kufanya kazi kwa bidii na kusonga mbele
Tuna tiwa nguvu na maneno ya mungu na ndio jibu kuhusu kupenya dhidi ya “”hofu”
MUHUBIRI 5:18-19
18 Tazama, mimi niliyoyaona kuwa ndiyo mema na ya kufaa, ni mtu kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote anayoifanya chini ya jua, siku zote za maisha yake alizopewa na Mungu; maana hilo ndilo fungu lake.
119 Tena, kwa habari za kila mwanadamu, ambaye Mungu amempa mali na ukwasi, akamwezesha kula katika hizo, na kuipokea sehemu yake, na kuifurahia amali yake; hiyo ndiyo karama ya Mungu.
Fanya kazi kwa bidii