PENZI LA MASHAKA

A STORY SCRIPT 

            BY

 SEBASTIAN S. MASABHA.

 0758-162527


SEHEMU YA PILI 02.

EXT: SEBBY ANAKAMATA SPANA NA KUANZA KUSHUSHA INJINI YA GARI.

SEBBY.

Dah! Hii ngoma nzito kweli kweli. Yaani hizi kazi za kuvamia huwa ni kipengele. Mtu unasomea jambo A unakuja kuhangaika na jambo B. tofauti kabisa na uhalisia.

{Sebby anashtushwa na ujio wa Konki ambaye anamgusa Sebby begani}

KONKI.

Vipi chafu yao, mbona unalonga mwenyewe asubuhi, asubuhi. Shida nini au ndo mastresi ya maisha?

SEBBY.

Aah! Wapi konki, maisha si ndo hayahaya tu mzee.

KONKI.

Sema bora yenu nyinyi mlioenda hata maskuli, maana mkipata gepu mchezo unageuka chapu kwa haraka.

SEBBY.

Sidhani mzee wangu, siyo kwa karne hii, labda Mungu atende miujiza.

KONKI.

Sema kweli, ila mimi naamini utatoboaga tu huko mambele, Jah atablesi.

SEBBY.

Shukrani buda, tuzidi kuombeana tu. Sema nini Konki embu nielekeze jambo kidogo hapa kwenye hii injini. Sijui kuna nati sijaifungua ama vipi.

KONKI.

Poa chafu yao, alafu leo Red vipi mbona sijamsoma mpaka sasa.

SEBBY.

Asee.. mwamba jana si kaguswa kidole na “Nge”

{Wakati Sebby na Konki wakiendelea na majukumu pamoja na maongezi yao. Anaingia Master gereji na vijana wake wengine}

MASTER.

Sasa chafu yao, wewe na masuala ya kutengeneza injini ni wapi na wapi. Nenda kazibe pancha kwenye lile gari jeupe. Hizi kazi zina wenyewe bhana.

{Sebby aliyefahamika kwa jina la chafu yao pale gereji, alikubali kwa kitikisa kichwa na kusimama kinyonge kwenda kufanya shughuli ya kuziba pancha ya gari jeupe}

MASTER.

Haya kila mmoja achakarike na sehemu yake sitaki vijana wazembe hapa, alafu tuje kusumbuana mda wa kukatiana jax (pesa). Yaani sitaki kabisa.

WOTE.

Sawa master tumekuelewa. Sisi ni nani hasa hadi tukupinge.

{Master gereji alikuwa ni moja ya watu wenye kupenda sifa, kuogopwa na kuheshimiwa kila mara kitendo ambacho kilikuwa kikiwanyima wafanyakazi wengine uhuru na kukaa vikundi kumsimanga}

Fade out

 

NJIRO NYUMBANI KWA KINA SABRINA (ASUBUHI)

{Sabrina msichana anayeishi maisha ya kishua anajaribu kutafakari na kujiuliza endapo kama kuna tofauti yoyote iliyojitokeza baina yake na Sebby}

SABRINA.

Hivi ni kitu gani kibaya nilichomfanyia sebby? Maana amebadilika ghafla tu, ona sasa hata sms zangu hataki kujibu.

{Mawazo ya Sabrina yanakosa majibu sahihi na subra. anaamua kumtumia Sebby ujumbe mwingine}

(Sabrina sms)

“Hey! Sebby mbona umechange sana now days, kama kuna kitu nimekukosea si bora uniambie maana nashindwa hata kukuelewa. Anyway naomba unijibu tafadhali”

{Ujumbe alioutuma sabrina unaonyesha kupokelewa na Sebby hivyo sabrina anashusha pumzi zake na kusubiria kwa hamu reply kutoka kwa Sebby}

(Sebby sms)

“..............................................................................................”

{Sabrina akiwa amejilaza kitandani. Anaamua kuyakimbiza macho yake kwenye simu baada ya kusikia mlio wa sms}

SABRINA.

Camong! Huyu mwanaume ananitumia sms hewa. OMG! What is this?

{Sabrina anashtuka na kuchukia baada ya kupokea sms hewa kutoka kwa Sebby. Lakini kwa sababu anampenda, haishii hapo bali anaendelea kufikiri ni kipi kingine cha kufanya}

SABRINA.

Jamani huyu Gentleman mbona ananifanyia hivi si ataniuwa kwa presha. Au nimtumie Sms nyingine?. But no....  atazidi kuniumiza coz atahisi nampenda sana. Eeeh! Ngoja nimpigie simu.

 {Sabrina anaona njia nzuri ya kupata majibu sahihi na kuutuliza moyo wake ni kumpigia Sebby}

SABRINA.

Yani huyu mwanaume sijui amekuaje, mbona simu yake inaita tu hata hapokei.

{Sabrina anajaribu kupiga tena simu huku akiwa na shauku kubwa ya simu yake kupokelewa}

SABRINA.

Jamani mbona hivi, ananifanyia makusudi au ndo ubize. Camong Sebby.

{Sabrina anachukia na kuirusha simu yake kisha anajilaza kitandani baada ya Sebby kutopokea calls zake}

Fade out.

 

GETONI UNGA LIMITED ( ASUBUHI)

INT. RED ANAAMKA KITANDANI.

{Red anaamka baada ya kumulikwa na mwanga wa jua uliokuwa ukipita katika upenyo wa dirisha}

RED.

Tobaa... kumbe kumeshakucha kiasi hiki wacha niamke kwanza alafu mafaili yatajipanga yenyewe kichwani.

{Kabla ya kufanya chochote kile Red anaangalia mkono wake kwenye sehemu aliyong’atwa na “Nge” usiku wa mawio hiyo}

RED.

Hapa mbona safi tu. Ila ngoja kwanza nikalambe supu yetu ya mtaa kwa mama mboksinyo alafu mafaili yataendelea kujipanga yenyewe kichwani.

{Red anatoka nje kuelekea mgahawani huku mswaki wake ukiwa mdomoni na mkono wake ukibeba kijichupa cha maji}

Fade out

 

MGAHAWANI (PAMBANA NA HALI YAKO MGAHAWA)-ASUBUHI

INT. RED ANAINGIA MGAHAWANI.

{Red anaingia mgahawani huku akipokelewa kwa mbwembwe na mama mboksinyo pamoja na baadhi ya marafiki zake}

MAMA MBOKSINYO.

Oyoooo...! Chali wa mapesa, chali wa kuvunja ndo huyo sasa anaingia mjengoni

RED.

Kausha basi Bi mdashi. Mbona unanukia wenge kama vile umemuona bakhresa kumbe kapuku mmoja tu.

MAMA MBOKSINYO.

Ahaah! Red kwa hiyo unanitolea nje siyo

RED.

Siyo nakutolea nje, tatizo lako uko resi sana yaani kelele nyingi wewe mama. mara mjengo, mjengo kuna mjengo hapa au kijimgahawaha tu.

{Mama mboksinyo mmiliki na muuza mgahawa wa pambana na hali yako anambadilikia Red ghafla baada ya kuona wanapishana lugha}

MAMA MBOKSINYO.

Embu tuyaache hayo maana ushanikasirisha Red. Kwanza nakudai buku, jana umekuja hapa umekula na kuondoka na mihogo bila ya kulipa.

RED.

Aaah! Bi mdashi ina maana wewe haujawahi kutaniwa?. Mimi na wewe tena, mbona hatujawahi kupingana wala kushindwana hiyo nitakulipa tu.

MAMA MBOKSINYO.

Siyo utanilipa ndo ulipe sasa. Kwanza unakula nini maana supu ya miguu ya kuku ndo inaishia-ishia hivyo

RED.

Aaah! Bi mdashi embu nifanyie maajabu mapema mambo yasije yakaharibika maana hapa nahisi kama vile tumbo linacheza singeli..

{Maneno ya Red yanawafanya watu wote walioko mgahawani kucheka wakati huo mama mboksinyo anamtengea Red supu ya miguu ya kuku}

MAMA MBOKSINYO.

Supu ya moto sana hii na ina pilipili ya kutosha ngoja nikuletee na kijiko.

RED.

Kijiko chako cha nini wakati unajua kila siku nakujaga ni kijiko changu.

MAMA MBOKSINYO.

Alafu wewe na nyatunyatu ndo mnaoongoza kuniibia vijiko vyangu hapa mgahawani maana kila siku lazima vijiko viwili ama vitatu vipotee.

RED.

Sinaga hizo pigo Bi mdashi, kwanza kijiko changu nimekichora tatoo.

{Red anaingiza mkono mfukoni na kutoa kijiko chake lakini kwa bahati mbaya mswaki aliouficha mfukoni nao unadondoka}

MAMA MBOKSINYO.

Jamani yaani haujawahi kuishiwa na maajabu kabisa ona sasa unaficha hadi mswaki mfukoni. Alafu nikisema unaniibiaga vijiko vyangu unaanza kuwaka.

Fade out.

GEREJI SINONI DARAJA MBILI (MCHANA)

EXT. SEBBY ANAPAMBANIA KOMBE.

{Sebby anahangaika kuziba pancha ya tairi la lori huku jasho zito likimtoka, nayo njaa ikiwasha moto ndani ya tumbo lake}

SEBBY.

Dah! Ama kweli maandiko hayajawahi kudanganya hata siku moja. Nimeamini wanaume tutakula kwa jasho.

{Baada ya njaa kali kumkabili sebby anaamua kumkopa konki elfu moja walau akapate chochote kitu kwenye duka lililopo pembezoni mwa gereji}

SEBBY.

Oya dingi naona hali ya tumbo haishikiki yaani hapa nahisi njaa changanya na kiu alafu sina hata mia ya kusingiziwa hivyo naomba uniazime buku nitakuvunjia badae tukishapatiwa vijisenti vyetu.

KONKI.

Poa chafu yao ila hakikisha unafanya kweli hapo badae maana nadaiwa bili ya maji maskani yaani mambo si mambo.

SEBBY.

Poa mkali nitahakikisha.

{Sebby akiwa mwingi wa mawazo na mwenye huzuni ya moyo anajifuta jasho na kusogea mpaka kwenye duka la mangi kununua juice na skonsi}

SEBBY.

Yaani kila nilifanyalo naona ni maseke tu. Madeni kila upande siyo kodi ya nyumba siyo chakula cha asubuhi, mchana wala usiku.

{Sebby anafika kwenye duka la mangi lakini anaweka mfukoni buku yake aliyopewa na konki na kujaribu kumkopa mangi}

SEBBY.

Niaje broh! Mangi

MANGI.

Poa vipi chafu yao.

SEBBY.

Fresh tu kaka mkubwa.

MANGI.

Nipange mzee wa kazi

SEBBY.

Ebhanaee.. ndungu yangu hapa niko apeche alolo alafu nina nenge hatari kama hautojali unikopeshe juisi ya jero na skonsi kesho nitakuletea pesa yako

MANGI.

Poa ila ufanye kweli si unajua hii ni biashara mzee.. alafu Juisi na skonsi mbona ni mbingu na ardhi kwa kazi unayoifanya, si sawa na kumkabidhi kichaa rungu.

SEBBY.

Dah! Sasa nitafanyaje kaka Mkubwa, wewe mwenyewe si unaona namna mazingira  yalivyokaa kishingo upande.

MANGI.

Basi poa chafu yao.

SEBBY.

Shukrani kaka

{Sebby anabeba juisi na skonsi yake kisha anarejea kibaruani lakini baada ya hatua tatu anapokea ujumbe wa simu kutoka kwa mpenzi wake stella}

(Stella sms)

“Hivi wewe mwanaume mbona kama nakubembeleza sana yaani mpaka sasa haujanitumia pesa ya kusuka na shughuli yenyewe imekaribia”

{Sebby anasikitika na kitikisa kichwa chake kisha anaamua kurudisha majibu ya ujumbe wa stella}

(Sebby sms)

“Jamani mpenzi wangu, wewe mwenyewe unanijua kwamba sijawahi kuremba mwandiko nikiwa nacho ila ukiona kimya ujue bado mambo hayajakaa sawa”

(Stella sms)

“Kwa hiyo unategemea mimi nifanyaje sasa”

(Sebby sms)

“Naomba nipe muda kidogo nishughulikie suala lako tafadhali”

{Sebby anamjibu stella ilimradi kumridhisha tu kwani mpaka wakati huo hakuwa na pesa nyingine zaidi ya buku aliyoazimwa na stella}

SEBBY.

Ila huyu mwanamke atakuja kunipa presha bure yaani laiti angelijua hali niliyo nayo kwa sasa asingelithubutu kuniomba hata mia

{Sebby anajilaumu mwenyewe mara ghafla apokea ujumbe mwingine wa simu kutoka kwa stella lakini anasita kuusoma na kaamua kuizima simu yake}

Fade out.

 

NJIRO NYUMANI KWA KINA SABRINA (MCHANA)

INT. SABRINA ANASHINDWA KULA CHAKULA.

Kutokana na kugubikwa na mawazo yaliyojaa hisia ndani yake sabrina anashindwa kula chakula cha mchana.

SABRINA.

Ila mapenzi upofu jamani yaani pamoja na utajiri wote tulionao hapa kwetu ndo mimi huyu nimenasa hivi kwa huyu mwanaume.

{Sabrina anachukua simu yake na kumpigia Sebby na wala asifanikiwe}

SABRINA.

Looh! Ndo ameamua kunizimia na simu jamani

{Sabrina anajiegemeza kitandani mwake kwa muda kidogo na baada ya dakika mbili simu yake inaita naye kwa bashasha anawahi kuipokea akijua ni sebby kumbe hapana}

SABRINA.

Hovyoo.. yaani huyu naye sijui hata nimwambiaje anielewe maana simtaki hata bure na kile kitambi chake.

{Sabrina anaamua kukata simu aliyopigiwa baada ya kupata wazo la kufanya kwa wakati huo juu ya sebby}

SABRINA.

Pengine Sebby hana salio kwenye simu yake ndo maana amenikaushia .

{Sabrina anaamua kuvuta kiasi cha laki moja na nusu kwenye simu  kutoka kwenye akaunti yake ya benki na kumtumia sebby laki moja}


ITAENDELEA....

N.B- USISAHAU KUDONDOSHA COMMENT YAKO NI MUHIMU

PIA USIKOSE KUFUATILIA MIENDELEZO YA TAMTHILIYA MBALIMBALI KUTOKA KWA MTUNZI NA MWANDISHI SEBASTIAN S MASABHA

 

1.PESA ZA SHEMEJI

2. KONEKSHENI ZA VALENTINE

3. SUKARI YA KIJIJI